Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki akomba tuzo ya tatu

Aziz Ki Simba Yanga Aziz Ki mchezaji Bora.

Sun, 5 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki, ameteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Aprili 2024 ndani ya Ligi Kuu ya NBC ikiwa ni tuzo yake ya tatu msimu huu katika ligi hiyo, lakini pia ni ya pili mfululizo baada ya mwezi Machi kuwa mshindi.

Aziz Ki amewashinda Joseph Guede wa Yanga na Kipre Junior (Azam) alioingia nao fainali kwenye mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa mwezi Aprili, Aziz Ki alionesha kiwango kikubwa na kuwa msaada kwa timu yake katika ushindi wa michezo mitatu kati ya minne ambayo timu hiyo ilicheza, hivyo Yanga kukusanya alama 10 na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi.

Yanga katika mwezi Aprili, ndani ya Ligi Kuu ya NBC matokeo yao yalikuwa hivi; Singida Fountain Gate 0-3 Yanga, Yanga 2-1 Simba, Yanga 1-0 Coastal Union na JKT Tanzania 0-0 Yanga.

Rekodi zinaonesha kwamba, tayari tuna tuzo nne za Mchezaji Bora wa Mwezi Ligi Kuu ya NBC msimu huu zilizobebwa na Maxi Nzengeli (Agosti 2023) na Aziz Ki (Oktoba 2023, Machi 2024 na Aprili 2024).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live