Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki akiondoka ni mtego huo

Pacome X Aziz Ki Majeruhi.png Aziz Ki akiondoka ni mtego huo

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alipoondoka mfalme wa Yanga SC (MVP) Fiston Mayele kauli hizi zilizojawa na furaha zilisikika kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa soka na wachambuzi nchini Tanzania.

"Yanga kwisha habari yao. Mayele ndio alikuwa Yanga, watamaliza wa (3) ligi kuu," hayo yalikuwa maneno yao.

Baada ya Mayele kuondoka :

◉ Yanga imekuwa tishio zaidi, Aziz Ki tayari ameyafikia magoli aliyofunga Mayele akiwa na mechi (2) mkononi, ndiye mfalme mpya aliyemrithi Mayele pale Jangwani anakaribia kuwa (MVP) wa ligi kuu (NBC).

◉ Yanga wametwaa Ubingwa wa ligi kuu mapema zaidi ya msimu uliopita

◉ Yanga wamefunga magoli mengi zaidi kuliko ile Yanga ya Mayele. Magoli yanafungwa na wachezaji tofauti tofauti.

◉ Yanga SC imetinga robo fainali CAF champions league baada ya miaka 25. Yanga imepiga pasi nyingi kuliko msimu uliopita. Yanga imekuwa tishio kuliko ile ya Mayele.

Kauli zimeanza tena:

"Aziz Ki akiondoka Yanga watapoteana. Aziz Ki ndio kila kitu Yanga akiondoka Yanga atashika nafasi ya (3) ligi kuu."

Mtego huo;

Nawakumbusha kuna mtu anaitwa Pacome Zouzoua (MVP) wa Ivory Coast huyu anaenda kuwa hatari zaidi ya Aziz Ki kwa sababu next season atakuwa kazoea mazingira ya Tanzania ni kama ilivyokuwa kwa Aziz Ki katika msimu wake wa kwanza.

24|25 huenda akawa mfalme mpya wa Young Africans Sports Club akimrithi Aziz Ki iwapo akiondoka. Ni ile falsafa ya 'Kata mti panda mti' ndiyo inatumika hapo Jangwani.

Wachezaji muhimu zaidi pale Yanga ambao wakiondoka Yanga itayumba ni (GSM) na Engineer Hersi Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live