Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki aachiwa msala Yanga

Aziz Ki Vs Prisons.jpeg Kiungo wa Yanga, Stephen Aziz Ki

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amependekeza majina ya mastaa saba kupewa muda wa mapumziko kutokana na kutumika zaidi, huku akisisitiza Stephen Aziz Ki ndiye atakayeiongoza timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023.

Yanga inatarajia kuanza mechi ya kwanza ya Mapinduzi dhidi ya KMKM siku ya Januari 4 mwakani. Nabi amemtaja Fiston Mayele, Yanick Bangala, Khalid Aucho, Dickson Job, Kibwana Shomari, Jesus Moloko na Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuwa ni wachezaji ambao wametumika zaidi hadi sasa hivyo wanatakiwa kupumzishwa kwaajili ya kuiweka miili sawa.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo kimesema wachezaji hao hawatakuwa miongoni mwa mastaa watakaocheza mechi ya kwanza ya Mapinduzi kutokana na nafasi ya mapumziko waliyopewa na kocha.

“Mfano Mayele akimaliza mechi na Mtibwa Sugar atakuwa na safari ya kwenda Congo kwaajili ya kufuatilia hati yake ya usafiri (pasipoti) ambayo imeshakwisha muda wake na Yanga ina mashindano ya kimataifa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

Djuma Shaban ataitumia kurudi katika makali yake.

Chanzo: Mwanaspoti