Wachezaji wote ambao ni wa Kimataifa walioko kwenye majukumu ya timu zao za Taifa wanatarajia kurejea nchini kabla ya Marchi 27 na kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa Jumamosi hii, Marchi 30, 2024.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari leo Marchi 25, 2024, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema, wachezaji hao wanatarajia kupata mazoezi kwa siku mbili hadi tatu kabla ya mechi ya Mamelodi.
"Wachezaji wote walioko kwenye majukumu ya timu zao za Taifa kwa maana ya Mali, Burkinafaso, Zambia Kenedy Musonda na Pacome tarehe 27 tunatarajia wote watakuwa wameshaingia jijini Dar kama kuna kuchelewa haitazidi tarehe 28," alisema Kamwe.