Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki: Hatuna presha na Mamelodi sisi

Aziz Ki 3029 Facebook Aziz Ki

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Stephanie Aziz Ki amesema hawana presha na mchezo ujao dhidi ya Mamelodi Sundowns kwani wamejiandaa vizuri kuanzia benchi la ufundi na wachezaji kuhakikisha wanapata matokeo chanya kwenye mchezo huo muhimu kwao.

Aziz amesema hayo kuelekea mchezo huo wa robo fainali ya CAFCL utakaopigwa kesho Ijumaa katika Dimba la Loftus Versfeld mjini Pretoria nchini Afrika Kusini baada ya ule wa kwanza uliopigwa katika Dimba la Mkapa Dar es Salaam weekend iliyopita kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

“Mechi itakuwa ngumu lakini Yanga tuna nafasi ya kufanya vizuri na kama tutapata matokeo basi yawe ya mapema kuwafanya wapinzani wawe na presha kubwa kutokana na matokeo ya mchezo uliopita, kurejea kwa wenzetu waliokuwa majeruhi ni faida kwa kikosi chetu na tutahakikisha tunawafurahisha mashabiki waliosafiri na wale ambao tumewakuta Afrika Kusini.

“Hatuna presha tutacheza na Mamelodi tukiwa na malengo ya kutaka kufuzu, tumeshacheza nao tunawajua, tulipokuwa nyumbani tulifanya makosa ya kutotumia nafasi lakini ugenini tutafatuta bao au mabao ili kuwaweka kwenye presha wapinzani wetu,” amesema Aziz Ki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live