Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki, Diarra kuwagawa mashabiki Yanga

Diara Na Aziz.png Aziz Ki, Diarra kuwagawa mashabiki Yanga

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Leo ndio leo. Nyota wawili wa Yanga, Stephane Aziz Ki wa Burkina Faso na kipa Djigui Diarra wa Mali leo watakuwa mahasimu wakati watakapokuwa wakizipambania timu zao za taifa katika mechi ya 16-Bora ya Afcon na mmoja wao lazima aage.

Mali ilitinga hatua hii ya mtoano baada ya kuongoza Kundi E ikiwa na pointi 5 ikifuatiwa na Afrika Kusini (pointi 4) na Namibia (pointi 4) ambazo zote zilifuzu 16-Bora na kuiacha Tunisia pekee ikiwa na pointi 2 mkiani.

Diarra alicheza mechi zote tatu za hatua ya makundi na kuruhusu bao moja tu, lakini jambo ambalo sio jema ni kwamba wao walifunga mabao matatu tu katika mechi tatu.

Watakutana na wa Burkinabe katika mechi itakayoanza saa 2:00 usiku, baada ya chama hilo la Aziz Ki kutinga 16-Bora likishika nafasi ya pili kundi D kwa pointi 4, nyuma walikuwa vinara Angola waliomaliza na pointi 7, huku wakiwa tayari wameshatangulia kwenye robo fainali baada ya kuing’oa Namibia kwa kuifunga 3-0. Timu nyingine katika kundi hilo zilikuwa Mauritania (pointi 3) na Algeria iliyoshika mkia ikiwa na pointi 2.

Mechi ya leo inatarajiwa kuwa na ushindani mkali na kuwagawa mashabiki wa Yanga ambao wengine watamshangilia Aziz na wengine Diarra, kwani timu hizo zinaonekana kulingana kiwango katika mechi zao za makundi, kama ilivyo Burkina Faso, Mali pia ilifunga mabao matatu na kuruhusu moja tu katika hatua ya makundi.

Lakini rekodi zinaonyesha, Mali na Burkina Faso zimekutana mara 6 tangu 2004. Kati ya hizo, Mali imeshinda 4, Burkina Faso imeshinda 1, na zimetoka sare mara moja. Kama rekodi zina maana yoyote leo, basi Aziz Ki atatangulia kurudi Jangwani, lakini soka haliko hivyo. Anaweza kutangulia kurudi Diarra. Sio ya kukosa kutazama hii.

Mechi nyingine ya leo itawakutanisha mabingwa wa mwaka 1976, Morocco dhidi ya mabingwa wa mwaka 1996, Afrika Kusini itakayochezwa kwenye Uwanja wa Laurent Pokou uliopo San Pedro kuanzia saa 5:00 usiku.

Chanzo: Mwanaspoti