Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki, Bangala warejea na moto Yanga

Aziz Ki Excl Aziz Ki

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Young Africans Sports Club Stephane Aziz Ki amemaliza adhabu ya kukosa mechi tatu sasa akiwa tayari kurejea kikosini kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kesho Jumamosi, Novemba 26, 2022.

Aziz Ki ambaye alipewa ruhusa kwenda kuitumikia timu ya Taifa, alikosa mechi dhidi ya Kagera Sugar, Singida Big Stars na Dodoma Jiji.

Fundi huyo mwenye mabao mawili katika ligi kuu ya NBC msimu huu, mlinda kango Djigui Diarra na Gael Bigirimana wamerejea kutoka kwenye majukumu ya timu Bigirimana.

Bigirimana alikuwa sehemu ya wachezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa mkoani Singida juzi.

Yannick Bangala anarejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kadi tatu za njano. Bangala alikosa mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live