Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI ndio darasa la namba 10 anavyopaswa kucheza

Aziz KI Stephen Gg Aziz KI ndio darasa la namba 10 anavyopaswa kucheza

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Achana na goli zake za kila siku ila leo tuzungumzie uwezo wake wa kupiga pasi ya mwisho “That pass”

Kusema ukweli huyu jamaa anatoa shule jinsi ya kuachia pasi ya mwisho na kumfanya mshambuliaji afunge kirahisi huku akiwa Onside.

Aziz KI kabla ajaachia pasi ya mwisho anamtazama mshambuliaji wake akifanya mikimbio ya kwenda mbele kisha anatazama ukuta wa wapinzani,halafu anaufyonza ule mpira kwa sekunde kadhaa na kuachia pasi blind side, kitu ambacho ni kigumu walinzi kumzuia mshambuliaji alie pigiwa pasi.

Rejea assist yake kwenda kwa Guede dhidi ya Belouizdad,tazama pasi yake ya leo kwenda kwa Muda kwenye goli la kwanza,rejea mechi ya 5-1 dhidi ya Simba na mechi kibao zilizopita utagundua hilo.

That Pass….ile pasi ya La pausa kutoka kwa mwamba wa Ouagadougou Aziz Ki ni motoo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: