Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI mfungaji Bora wa NBCPL 2023/24

Aziz Ki Afq4w.jpeg Aziz KI mfungaji Bora wa NBCPL 2023/24

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki ametangazwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2023/24.

Aziz Ki aliibuka kinara wa upachikaji magoli akiingia kambani mara 21 magoli mawili mbele ya nyota wa Azam Fc, Faisal Salum ‘Feitoto’ aliyemaliza na magoli 19.

Nafasi ya tatu inashikiliwa na Wazir Junior (magoli 12), Saido Ntibanzokiza mwenye magoli 11 sawa na Maxi Nzengeli (magoli 11).

Aziz KI ameibuka kinara wa kubeba awards nyingi zilizotokana na msimu bora aliokuwa nao ikiwemo MVP wa msimu.

Aziz Ki ametwaa tuzo tatu katika usiku wa tuzo za TFF (NBC PL)

1: Mfungaji bora

2: Kiungo bora

3: Mchezaji bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live