Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI awapa 'Thank You' Wananchi; "Asanteni katika kipindi chote"

Aziz Mashabiki Mz Aziz KI

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Stephanie Aziz Ki raia wa Ivory Coast amewashukuru mashabiki wa timu hiyo maarufu kama Wananchi kwa sapoti kubwa ambayo wamekuwa wakimpa yeye pamoja na wachezaji wenzake wote kwa msimu mzima.

Aziz KI amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kuelekea mchezo wa mwisho wa kutamatisha Ligi Kuu ya NBC ambapo mechi zaote zitapigwa huku Yanga wakitarajiwa kucheza na Tanzania Prisons katika Dimba la Chamazi Complex majira ya saa 10.

"Mechi ya mwisho ya msimu huu kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema yake na napenda kuwashukuru familia yangu, wachezaji wenzangu, wakufunzi, wafanyakazi na uongozi wa Yanga.

"Lakini kubwa zaidi, nasema asanteni sana mashabiki wa Wananchi kwa sapoti katika kipindi chote cha ligi. Nakiri kuwa hakuna kilichokuwa rahisi ila mlikuwepo kunisukuma, kunifanya niwe bora na kunipa kila lililo bora.

"Kwa mara nyingine nasema tena asanteni kwa sapoti na upendo wenu kwangu natumai msimu ujao utakuwa maajabu mengine kwetu inshallah #ksa10⚽️ #chanya kila wakati."

"Last match of the season I would first like to say thank you to GOD Almighty for his grace and I would love to Thank my family, my teammates, coaching staff, staff and the management of Yanga but most importantly, Thank You to the fans of wananchi for the support throughout the league I admit that nothing was easy but you were there to push me to surpass and always give the best of me once again thank you for your support and love towards me I hope that next season will be another marvel for us inshallah. #ksa10 ⚽️

Aziz ndiyo kinara wa mabao ndani ya Yanga huku pia akilingana na Fei Toto wote wakiwa na mabao 18 na leo ndiyo siku itakayoamua nani atakuwa mfungaji Bora wa Ligi Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live