Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI amuibua kocha Mfaransa

Aziz KI Mpira Aziz KI amuibua kocha Mfaransa

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz KI yuko kwenye kiwango bora msimu huu na sasa ubora huo umemchongea kocha wa Timu ya Taifa ya Burkinafaso, Hubert Velud.

Kocha Velud amejikuta kwenye presha kubwa juzi wakati akitangaza kikosi cha taifa akikaliwa kooni juu ya matumizi ya Aziz KI anapojiunga na timu ya taifa hilo.

Iko hivi mashabiki wa Burkinafaso huwambii kitu kuhusu Aziz KI hasa baada ya staa huyo kuchagua kulitumikia taifa hilo badala ya Ivory Coast ambako familia yake inakaa.

Mashabiki wa soka nchini humo wamekoshwa na kiwango cha Aziz KI msimu huu akiwa na Yanga ambapo juzi walimganda kocha huyo raia wa Ufaransa wakitaka wajue kwanini kiungo huyo haanzi kwenye timu ya taifa.

Msimu huu Aziz KI amekuwa kwenye moto akiwa tayari anaongoza kwenye msimamo wa wafungaji akifunga mabao saba kwenye Ligi Kuu Bara.

Kocha Velud ameliambia Mwanaspoti hana shida na kiungo huyo na kwamba presha ya mashabiki wa taifa lake inampa changamoto kiungo huyo kupandisha ubora wake hata anapojiunga na timu ya taifa hilo.

Velud alikiri kuimarika kwa Aziz KI msimu huu akiwa na Yanga na amekuwa pia kwenye mawasiliano mazuri na makocha wa klabu yake kuhakikisha wanasaidiana kumuimarisha kiungo huyo.

“Kazi yetu kama makocha ni presha wakati wote, najua kiu ya mashabiki wanatamani kuona wachezaji wao wote sio tu KI (Aziz) wanacheza kwa ubora timu ya taifa kama ambavyo wanajituma klabuni kwao,” alisema Velud ambaye aliwahi kukaribia kufanya kazi Simba na Yanga katika nyakati tofauti.

“Tangu nianze kazi hapa nimekuwa kwenye mawasiliano bora na makocha wa Yanga Nasreddine (Nabi) na sasa nataka kuzungumza na huyu wa sasa (Miguel Gamondi) lengo ni kutaka kuona anaendelea kuwa bora, ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na sasa yuko sawasawa zaidi.”

Aziz KI alimaliza msimu ulioisha vibaya huku baadhi ya mashabiki wa Yanga wakiaamini kwamba hakustaili kuendelea kuitumikia klabu yao.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: