Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI amkaribisha Prince Dube Yanga

Chama Aziz Dube Aziz KI amkaribisha Prince Dube Yanga

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama alivyofanya kwa Clatous Chama, kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amemkaribisha Prince Dube 'Mwana Mfalme' ambaye Yanga ilithibitisha kukamilisha usajili wake usiku wa kuamkia Jumapili.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Aziz Ki aliweka chapisho la kumkaribisha Dube huku akimtaja kama mfungaji bora wa Ligi Kuu 2024/25 Ni wazi Aziz Ki alikuwa akisubiri kwa hamu utambulisho wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Azam Fc, akionekana kumkubali.

Aziz Ki alikuwa mchezaji wa kwanza kufichua usajili wa Dube katika moja ya mahojiano yake katika mitandao ya kijamii.

Aziz Ki aliweka bayana kuwa msimu ujao hana mpango na tuzo ya mfungaji bora kwani atahakikisha tuzo hiyo inabebwa na washambuliaji wa Yanga zaidi akimtaja Dube.

Msimu ujao Dube na washambuliaji wenzake katika kikosi cha Yanga washindwe wenyewe tu katika kuzifumania nyavu kwani kikosi kimesheheni wapishi wa kuwatengenezea nafasi.

Chama, Aziz Ki, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli wote watakuwa kazi moja tu, kuwatengeneza nafasi lakini pia hawataacha kufunga kama walivyofanya msimu uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live