Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI alivyoamsha shangwe Sokoine

Aziz KI Mpira Aziz KI alivyoamsha shengwe Sokoine

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kuchelewa kuwasili Uwanja wa Sokoine kwa dakika 10, Mashabiki wa Yanga wameamsha shangwe kwenye uwanja huo baada ya kumwona nyota wa timu hiyo, Stephen Aziz Ki.

Yanga imetua saa 8:22 ikiachwa na wapinzani wao Tanzania Prisons waliotangulia saa 8:12 mchana wakiingia kimyakimya bila shangwe hadi vyumbani.

Aziz Ki ambaye amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga, amekosekana katika michezo minne ikiwamo mmoja wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) akiwa na timu yake ya Taifa ya Burkina Faso kwenye michuano ya fainali za Afcon Ivory Coast.

Katika michezo hiyo aliyokosekana staa huyo, Yanga imeshinda mitatu ikifunga mabao manane na kuruhusu mawili ikifuzu 32 ya ASFC na kubaki kileleni Ligi Kuu kwa pointi 37 na suluhu moja dhidi ya Kagera Sugar.

Katika msafara wa kikosi cha Yanga kilichoingia uwanjani kwa eskoti ya gari la polisi, Aziz Ki alikuwa gari la mwanzo akiwa siti ya mbele na kuwafanya mashabiki kulipuka kwa shangwe.

Aziz KI kwenye michezo ya Yanga msimu huu amehusika na mabao 12 akifunga 10 na kuasisti mawili katika Ligi Kuu Bara huku nakiwa ndiye kinara wa mabao kwenye msimamo wa wafungaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: