Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI akitaka kiatu cha Mayele, Saido

Aziz KI Mpira Stephen Aziz KI

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanzoni mwa msimu huu hakuna aliyekuwa akimpigia hesabu na hata mwenyewe hakuwa na mpango kabisa wa kuwania kiatu cha Dhahabu cha Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara, lakini ghafla upepo umebadilika na sasa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki amesema anakitaka kiatu hicho.

Aziz Ki amepata jeuri hiyo baada ya kufunga bao la 10 kwa njia ya friikiki, wakati Yanga ikiizamisha Tabora United katika pambano kali la Ligi Kuu lililopigwa juzi usiku Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma na kumfanya nyota huyo kuvunja rekodi binafsi ya mabao aliyoiweka msimu uliopita alipofunga mabao tisa tu.

Tofauti na msimu uliopita alipofunga mabao hayo kupitia mechi 30 za msimu mzima, safari hii Aziz Ki amefunga 10 kupitia mechi 13 t, jambo lililompa mzuka mwingi na kusema sasa anataka tuzo ya Mfungaji Bora sambamba na kuhakikisha Yanga inatetea taji la ligi kwa msimu wa tati mfululizo.

Akizungumza na Mwanaspoti jana, nyota huyo raia wa Burkina Faso aliyeitwa pia timu ya taifa ya nchi hiyo, amesema haikuwa rahisi kuvunja rekodi hiyo binafsi ya mabao katika ligi, lakini anajivunia kucheza kwenye timu yenye kikosi bora cha ushindani, kwani imemfanya awe bora zaidi kuliko msimu uliopita.

“Kufunga mabao 10 kabla ya duru la kwanza kumalizika ni rekodi kubwa kwangu, kwa vile msimu uliopita nilifunga kwa msimu mzima mabao tisa, hii ni kutokana na ubora wa kikosi na muunganiko mzuri wa wachezaji ambao hakuna mchezaji anaetegemewa kila mmoja akipata nafasi anatakiwa kufunga,” alisema Aziz Ki na kuongeza;

“Ukiachana na hilo mimi nimekabidhiwa rungu na Kocha Miguel Gamondi aliyenitaka nihakikishe natumia vizuri nafasi ninazozipata akinipa kazi ya kuhakikisha namaliza msimu nikiwa mfungaji bora hivyo sasa ninachokifanya ni utekelezaji.”

Aziz Ki amesema ni rekodi nzuri kwake kuona anaendelea kuimarika na kufanya mambo makubwa ndani ya timu yake kwani kufikia rekodi ya msimu uliopita mapema kunampa picha ya kuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi huku akiweka wazi hilo linawezekana kutokana na aina ya kikosi walichonacho.

Amesema asipofunga idadi kubwa basi atahakikisha anakuwa mchezaji aliyehusika kwa idadi kubwa ya mabao yatakayofungwa na timu hiyo msimu huu kwa kutoa pasi za mwisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: