Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI aibuka mfungaji Bora, Fei Toto chali - Tazama mabao yote

Aziz Ki Mfungaji Bora Aziz KI aibuka mfungaji Bora, Fei Toto chali

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki ndiye Mfungaji Bora kwenye NBC Premier League msimu huu wa 2023/24 akiwa na jumla ya magoli 21.

Aziz Ki amefunga mabao matatu (hat-trick) kati ya mabao manne ambayo Yanga wameshinda kwenye ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

Aziz Ki amefikisha magoli 21 kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara mpaka mechi ya mwisho ya msimu huu huku aliyekuwa akifukuzana naye, Feisal Salum Abdallah akifunga bao moja dhidi ya geita kwenye ushindi wa mabao 2-0 na kufikisha mabao 19.

Kabla ya hapo nyota hao walikuwa wakilingana baada ya kila mmoja kufunga mabao 18.

Aziz amekuwa na msimu bora sana, na hii ni hat-trick ya pili kwa Aziz Ki msimu huu ambapo hat-trick ya kwanza alifunga dhidi ya Azam Fc kwenye mzunguko wa kwanza katika mechia ambayo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 3-2.

FT: Yanga 4-1 TZ Prisons (Aziz Ki 11’, 12’, 79’, Musonda 52’ / Ngasa 4’)



Full Time|

Simba 2-0 JKT Tanzania

Yanga SC 4-1 Tz Prisons

Geita Gold 0-2 Azam FC

Singida FG 2-3 Kagera

Mashujaa 3-0 Dodoma

Namungo 3-1 Tabora Utd

Coastal Union 0-0 KMC

Ihefu 5-1 Mtibwa Sugar.







Chanzo: www.tanzaniaweb.live