Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI aanika kila kitu Mobetto kumbakisha Yanga, amtaja mama yake

Video Archive
Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Stephanie Aziz Ki amesema kuwa ameamua kuongeza kandarasi yake ya kuendelea kusalia Jangwani kwa sababu ya mapenzi yake kwa mabingwa hao wa muda wote wa Ligi Kuu Tanzania na si kwa sababu ya kushawishia na mrembo Hamisa Mobetto kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakisema.

Aziz amesema hayo leo Alhamisi, Julai 18, 2024 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati kikosi cha Yanga kikiondoka kuelekea nchini Afrika Kusini kwa mwaliko maalum wa Kaizer Chiefs ajili ya maandalizi ya msimu ujao na mechi kadhaa za kirafiki ikiwemo michuano ya Kombe la Toyota.

"Soka ni soka wala hakuna mtu anayeweza kukufanyia maamuzi badala yako. Wakati nakuja kusaini nilikuja na mama yangu ambaye alisimamia kila kitu, kama kubaki niimebaki Yanga kwa sababu mapenzi yangu kwa timu wala sio kwa sababu ya Hamisa Mobetto, yeye ni rafiki yangu tu.

"Mashabiki wa wa Yanga wamenifanyia mambo makubwa, wamenipa sapoti kubwa tangu nimekuja Yanga na kunifanya niendelee kuwa bora zaidi.

"Najisikia furaha kucheza na Chama na Prince Dube ambao wamekuwa na misimu bora hapo nyuma ni furaha kuwa nao ndani ya timu moja, ni jambo jema kwa kuwa tutakuwa na muendelezo mzuri wa kucheza vizuri kwa kuwa tunakuwa na wachezaji wengi wazuri ndani ya timu,” amesema Stephane Aziz Ki.

Kwa upande wake, Mobetto amefafanua kuwa; "Hakuna mtu aliyenifuata akasema nimshawishi (Aziz Ki). Ni mchezaji mzuri sana ni vizuri kama kabaki Tanzania, angeondoka ningepanda ndege kumfuata. Nilimwambia asiondoke, ni mtu mzuri ana upendo."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: