Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI: Tanzania hakuna wa kuisumbua Yanga

Aziz KI Guard Of Honour.jpeg Aziz Ki.

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki amekiangalia kikosi cha timu hiyo na kudai kwa sasa kipaumbele chao ni kutafuta kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Akizungumza nasi, Aziz Ki amesema wamefanya vizuri katika mashindano ya ndani na sasa wanatakiwa kupambana na kuongeza nguvu zaidi katika michuano ya Kimataifa ikiwemo kucheza fainali ya Afrika.

“Kwa sasa kipaumbele chetu ni kucheza fainali ligi ya Mabingwa,kwa ligi ya ndani hakuna mpinzani. Nilikuwa sahihi kumuamini Rais Hersi Said kwa miaka hii miwili ya ajabu , Asante kwake sasa tusonge kileleni mwa Afrika.

Amesema kwa sasa viongozi wanatakiwa kufikiria na kuwekeza zaidi katika michuano ya Afrika, kwa kusonga mbele zaidi kucheza nusu hadi fainali ya michuano hiyo ambayo msimu huu wamefikia hatua ya robo kwa kuwa ndani tayari wamefanikiwa sehemu kubwa.

Aziz Ki ameonesha kiwango bora ndani ya kikosi cha Yanga kwa kusaidia timu hiyo kufanikiwa kucheza kombe la Shirikisho la Afrika msimu 2022/23 na kuipeleka timu hiyo makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya miaka 25.

Kwa sasa, Kiungo huyo yupo katika hatua za mwisho za mazungumzo na uongozi wa Yanga kwa ajili ya kuongeza mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo kwa msimu wa 2024/25.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live