Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI, Mayele ampa jeuri Nabi

Aziz Ki Y Aziz KI, Mayele ampa jeuri Nabi

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga sasa akili yote ni nchini Tunisia wakijiandaa kuwafuata wapinzani wao US Monastir, lakini kocha wao Nasreddine Nabi amefichua jeuri ya kikosi hicho kilichoshinda mechi tisa mfululizo ikiwa ni rekodi nchini, lakini kuna mapya yameibuka kwa Bernard Morrison 'BM33'.

Tangu ilipofungwa na Ihefu kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa Novemba 29 mwaka jana baada ya Yanga kushinda mechi 49, timu hiyo haijapoteza tena zaidi ya kushinda mechi tisa mfululizo ikiivunja rekodi ya Azam FC iliyoshinda mechi nane mfululizo msimu huu .

Akizungumza na Mwanaspoti Nabi alisema wakati wanajipanga na safari ya kuwafuata US Monastir katika mchezo wa kwanza wa makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ubora wao wa kupata matokeo bora kwenye ligi ni kielelezo cha ubora wa timu yao.

Nabi alisema, japo bado anakabiliwa na utofauti wa utimamu wa mwili wa mastaa wake hasa wanaotoka majeruhi, ila watatua Tunis kwa akili ya kupata matokeo bora, akiwataja Stephane Aziz KI, Fiston Mayele, Khalid Aucho, Kennedy Musonda, kipa Diarra Djigui kumpa jeuri.

Yanga itacheza na US Monastir Jumapili hii, huku kikosi hicho kikianza safari yake leo Februari 7 saa 9 alasiri.

"Kushinda kwetu nyumbani kwa mechi tisa mfululizo ni ishara kwamba tuliishi kwa malengo yetu ambayo yalianzia mbali sio tu hapa tulipofikia sasa," alisema Nabi.

"Ukiangalia katika timu za ndani tulijitofautisha na timu nyingi kuanzia uundwaji wa kikosi chetu, nafikiri Yanga inastahili heshima hata kwa usajili ambao tuliufanya kwa utulivu zaidi, hata kama tuna mapungufu sio mengi kulinganisha na timu zingine.

"Ukitoka hapo ubora wetu mwingine ukaongezeka kupitia programu ya mazoezi yetu, tuna wachezaji wanaojituma zaidi mazoezini hii imesaidia kuboresha ushindani wa mchezaji mmoja kwenda mwingine kwa nafasi, ndio maana hata akikosekana mchezaji mmoja inakuwa sio tatizo kubwa sana," alisema Nabi aliyewamwagia sifa nmyota wake wakisema wanajituma sana uwanjani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live