Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz KI, Fei Toto ni mtifuano mzito leo

Fei Toto Amfunika Aziz Ki Ligi Kuu Aziz KI, Fei Toto ni mtifuano mzito leo

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viungo washambuliaji Aziz Ki na Feisal Salum “Fei Toto” vita yao kwenye rekodi ilikuwa ngoma nzito kutokana na kila mmoja kupambana kufikia malengo yao kwa msimu wa 2023/24 na mwisho Aziz Ki alikuwa namba moja kwenye utupiaji akiwa na mabao 21 Fei mabao 19.

Wachezaji hawa wawili ambao waliwahi kucheza timu moja wakiwa Yanga, msimu uliomalizika walikuwa na takwimu nzuri sana ndani ya uwanja.

Aziz Ki ndiye aliyekuwa kinara wa ufungaji akiwa na mabao 21, huku nyuma yake akifuatiwa na Fei Toto akiwa na mabao 19, mchuano huu ulihitimishwa hadi mechi ya mwisho ya Ligi.

Katika tuzo za TFF kwa msimu wa 2023/24 wachezaji hawa wapo katika kinyang’anyaro kimoja cha Kiungo bora na Mchezaji bora wa Msimu. Usiku wa Tuzo za TFF ni leo usiku katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar Es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live