Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Andambwile kutua Yanga

Aziz Andambwile Az3uV Aziz Andambwile kutua Yanga

Tue, 9 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya dili la kumpata Yusuf Kagoma ili kuongeza nguvu eneo la kiungo kushindikana na nyota huyo kutambulishwa Simba jana, Yanga imejibu mapigo kwa kushusha kiungo mwingine atakayecheza nafasi hiyo.

Yanga ilikuwa ya kwanza kumfuata Kagoma aliyeitumikia Singida Fountain Gate msimu uliopita ili kumpa mkataba, lakini wakati ikiendelea kujadili juu ya ishu ya maslahi, Mafia wa Simba wakaingilia dili hilo na kumaliza mchezo mapema.

Baada ya Simba kukamilisha kila kitu jana ikamtambulisha na kuiacha Yanga ikishangaa na kuamua kuhamishia nguvu sehemu nyingine.

Hivi sasa inaelezwa kwamba Yanga haijakaa kinyonge kwani ilipoona mambo magumu kwa Kagoma, ikamvutia waya Aziz Andambwile na ipo katika hatua nzuri ya kumalizana. Kumbuka nyota hao wote msimu uliopita walikuwa Singida Fountain Gate wakicheza kikosi cha kwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live