Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azim Dewji: Mimi nilimkataa Robertinho kitambo sana!

Azim Dewji Kauli Azim Dewji: Mimi nilimkataa Robertinho kitambo sana!

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfadhili wa zamani wa Simba SC na mdau wa soka nchini, Azim Dewji, amesema yeye alikuwa mtu wa kwanza kumkataa Kocha Roberto Oliviera 'Roberthinho' kabla hajatimuliwa juzi.

Azim amesema, aliwahoji viongozi kuhusu suala hilo kwani alifahamu wazi kwamba malengo ya klabu kwa sasa sio kuingia Makundi Klabu Bingwa bali ni zaidi ya hapo.

“Niliwauliza viongozi wa Simba Sc huyu kocha ametoka timu gani wakaniambia ametoka Vipers ya Uganda, niliwaambia mbona Vipers ni timu ndogo sana sisi tunataka kocha mkubwa sio kocha wa kutoka kwenye timu ndogo sisi malengo yetu ni makubwa,” alisema Azim Dewji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live