Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yazidi kuiacha mbali Yanga kwenye msimamo

Azam Yazidi Kuiacha Mbali Yanga Kwenye Msimamo.jpeg Azam yazidi kuiacha mbali Yanga kwenye msimamo

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Azam FC imezidi kujikita kileleni kwenye msimamo na kuiacha mbali Yanga SC ambayo inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo.

Azam wamefanikiwa kufikisha alama 28 baada ya kuishushia kipigo cha 2-1 dhidi ya JKT Tanzania hapo jana Desemba 11, 2023 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.

Magoli ya Azam FC yalifungwa na Sospeter Bajana na Idd Seleman Nando huku goli pekee la JKT likifungwa na Najimu Magulu.

Yanga wamebaki nafasi ya pili wakiwa na alama zao 24 wakiwa na viporo vyao 3 mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live