Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yarejea mzigoni

Azam Pic Data Azam yarejea mzigoni

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KIKOSI cha Azam kimerejea mazoezini rasmi juzi Jumatatu  wakijiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo utakaochezwa Aprili sita katika uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.

Akizungumza na Mwanaspoti, Afisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria 'Zaka' alisema walisimama kufanya mazoezi tangu ulipotangazwa msiba wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli.

"Tulisimama mazoezi lakini Jumatatu jioni ndio tulirejea kuanza mazoezi kwa siku ya kwanza na leo Jumanne tutaendela na mazoezi".

Zaka alisema wakiwa wametoka kwenye mapuzmiko hayo wanaanza na programu ya kufanya mazoezi mara moja kwa siku tu kwanza.

"Hapana programu yetu itakuwa ni mazoezi jioni tu kwa mara moja, labda baada ya hapo ndio kunaweza kukawa na mabadiliko mengine".

Azam inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 44 katika mechi 24, wakishinda mechi 12 , sare nane na kupoteza mechi nne.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz