Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yapata ushindi wa kwanza Ligi Kuu

Azam Yashinda Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Azam FC imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Primia Ligi) msimu huu baada ya kuichapa Namungo FC 1-0 usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Ni bao la mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo dakika ya 90 lililompa pointi tatu za kwanza kocha Mzambia, George Lwandamina.

Azam FC inafikisha pointi nne katika mchezo wa tatu, ikitoka kutoa sare ya 1-1 na Coastal Union Jijini Tanga kabla ya kuchapwa 2-1 na Polisi Tanzania mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati Namungo FC inabaki na pointi tano kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Geita Gold kwenye mechi ya kwanza kabla ya sare ya 1-1 na Kagera Sugar zote Uwanja Ilulu mjini Lindi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live