Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yang'ara, Dodoma mambo bado Ligi Kuu

Azam Vs Dodoma Jiji Azam yang'ara, Dodoma mambo bado Ligi Kuu

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

TIMU ya Azam FC imetumia vyema uwanja wake wa Azam Complex baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1, dhidi ya Dodoma Jiji.

Mabao ya Azam yamefungwa na nyota wa kikosi hicho, Feisal Salum 'Fei Toto' aliyefunga mawili huku Ayoub Lyanga na Kipre Junior wakifunga moja kila mmoja wao wakati lile la Dodoma Jiji limefungwa na, Emmanuel Martin kwa mkwaju wa penalti.

Azam imepata ushindi huo baada ya kulazimishwa sare michezo miwili mfululizo ikianza na 0-0 dhidi ya Tabora United na 1-1 na Tanzania Prisons.

Matokeo hayo yanaifanya kuendelea kushikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi 43 sawa na Yanga ila zimetofautina mabao ya kufunga na kufungwa kama ilivyokuwa pia tofauti katika michezo ambayo hadi sasa zimecheza.

Katika michezo 19 ambayo Azam imecheza imeshinda 13, sare minne na kupoteza miwili huku kwa upande wa Dodoma Jiji iliyocheza mechi 18 imeshinda mitano, sare mitano na kupoteza minane na kuifanya kushika nafasi ya 12 na pointi zake 20.

Dodoma Jiji inayonolewa na Kocha Mkuu Mkenya, Francis Baraza inaifanya kutoshinda katika michezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu Bara tangu mara ya mwisho iliposhinda bao 1-0, dhidi ya Ihefu, mechi ikipigwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma Desemba 18, mwaka jana.

Chanzo: Mwanaspoti