Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yampa 'thank you' kocha Dabo na wenzake

Dabo Dsc Kocha Dabo

Tue, 3 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya wakurugenzi ya Azam FC na kocha Youssouph Dabo wamefikia makubaliano ya pande mbili ya kutoendelea kufanya kazi pamoja kuanzia leo Septemba 3, 2024.

Dabo aliyehudumu Azam FC kwa kipindi cha mwaka mmoja anondoka na wasaidizi wake watano wa benchi la ufundi aliokuja nao ambao ni kocha msaidizi Bruno Ferry (Ufaransa), kocha wa makipa Khalifa Babacar Fall (Senegal) kocha wa utimamu wa mwili Jean Laurent Geronimi (Ufaransa), mchambuzi wa video na wapinzani Ibrahim Diop (Senegal) na mchua misuli Ebrima Saine (Gambia).

Kuondoka kwa Dabo kunahitimisha mwaka mmoja wa utumishi wake ndani ya klabu hiyo, ulianza msimu uliopita.

Itakumbykwa kuwa, hivi karibuni Azam chini ya Dabo iliondolewa kwenye CAF Champions League na APR ya Rwanda katika hatua za awali kabisa na kabla ya hapo ilikubali kichapo cha bao 4-1 dhidi ya Yanga kwenye fainali ya Ngao ya Jamii licha ya usajili mzuri walioufanya msimu huu.

Aidha, msimu uliopita, Azm iliondolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika katika hatua za awali wakati kwenye ligi ikimaliza nafasi ya pili bila kutwaa taji lolote.

Rekodi za Dabo akiwa na Azam FC

1. Ligi Kuu

- Mechi 31

- ⁠Kushinda 21

- ⁠Sare 7

- ⁠Kupoteza 3

2. Kombe la Shirikisho la CRDB

- Mechi 6

- Kushinda 5

- ⁠Kupoteza 1

3. Kombe la Shirikisho la CAF

- Mechi 2

- ⁠Kushinda 1

- ⁠Kupoteza 1

4. Ligi ya Mabingwa CAF

- Mechi 2

- ⁠Kushinda 1

- ⁠Kupoteza 1

5. Kombe la Mapinduzi

- Mechi 4

- Kushinda 2

- ⁠Sare 1

- ⁠Kupoteza 1.

Bodi ya Azam FC ipo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya, kipindi hiki programu za timu zitakuwa chini ya makocha wa timu za vijana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live