Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yaleta neema viwanja Ligi Kuu Bara

AZAM.png Azam yaleta neema viwanja Ligi Kuu Bara

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author UONGOZI wa Azam Media umeleta neema katika Ligi Kuu Bara baada ya kutangaza kuweka taa katika baadhi ya viwanja vinavyotumiwa na klabu za Ligi Kuu.

Hayo yamesemwa na Injinia wa Azam Media, Frank Ndozero leo Jumanne Februari 16, 2021 wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Frank amesema baada ya kukaa chini na TFF pamoja na Bodi ya Ligi waliamua kuanza na viwanja vinne kuhakikisha vinawekwa mradi huo ili mechi ziweze kuchezwa usiku.

"Projekti hii ilianza mwezi wa nane mwaka jana, tulipita katika viwanja vya Majaliwa, Gwambina, Kaitaba na Mkwakwani kuona namna ambavyo tunaweza kuweka projekti yetu."

"Tunachoangalia cha kwanza ni sehemu nzuri ya kuchezea, nashukuru TFF wamekuwa bora sana kuhakikisha viwanja vinakuwa na sehemu nzuri ya kuchezea."

Frank alisema projekti hiyo ni mradi mkubwa ambao umechukua mabilioni ya pesa kuhakikisha unafanyika vizuri.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz