Uongozi wa Klabu ya Azam FC umeanza Mipango ya kuushawishi uongozi wa klabu ya Al-Merrikh juu ya kuipata huduma ya kudumu ya kipa wao Mohammed Mustafa ambaye amemaliza mkataba wake wa mkopo wa miezi 6.
Azam FC wamevutiwa na kiwango alichokionesha Mohammed Mustafa na kutaka kumnunua moja kwa moja.
Licha ya Klabu ya Al-Merrikh kuutarifu Uongozi wa Azam kuwa inamuhitaji kipa wao kuelekea msimu mpya ambapo klabu hiyo kutoka nchini Sudan itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu ya nchini Mauritania ila Uongozi wa klabu ya Azam nao umeonyesha Uhitaji Mkubwa mno na ndio maana mpaka sasa bado mazungumzo yanaendelea.
Takwimu za Mustafa akiwa Azam FC ligi kuu 2023|24:
Michezo 16
Clean sheets 8.