Baada ya kutolewa kwenye mashindano ya Mapinduzi Azam FC kwa kipigo cha mabao 4-1, Kaimu Ofisa Habari wa timu hiyo, Hashim Ibwe amesema kikosi chao kitaendelea kubaki visiwani Zanzibar hadi Januari 14.
Azam FC ambao ni mabingwa mara tano wa Mapinduzi wakitwaa msimu wa 2012 kwa kushinda mabao 3-1 Jamhuri, 2013 waliifunga mabao 2-1 Tusker FC, 2017 walishinda bao 1-0 Simba 2018 dakika 90 walitoka suluhu wakashinda kwa mikwaju ya penati (4-3) URA na 2019 iliikandamiza Simba mabao 2-1.
Akizungumza mara baada ya kipigo hicho Ibwe alisema wamesahau matokeo sasa wanajiandaa na mechi za ligi kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Zanzibar leo.
“Mpira ni mchezo wa makosa wachezaji wetu wamefanya makosa kocha ameyaona atayafanyia kazi kabla ya kuwakabili Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu bara.”
Alisema timu itaendelea kubaki hapa hadi Januari 14 na leo watakuwa na mchezo huo wa kirafiki maalum kwaajili ya kuendelea kukiimarisha kikosi chao ambacho.