Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yajitutumua kwa Geita, yaichapa bao 1

Kola Azam Mfungaji wa goli pekee la Azam FC

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji la Dar es Salaam, timu ya Azam FC,imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa Azam Complex Chamazi.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani wa hali ya juu uliwashuhudia Azam ambao mpaka wanakwenda katika mtanange huo wakiwa wameshinda mechi moja tu kati ya nne walizokuwa wamecheza wakisaka ushindi kila dakika ya mchezo.

Goli pekee la Azam na la ushindi katika mchezo huo,limewekwa kimiani na Rodgers Kola dakika ya 81 ya mchezo, kwa shuti zuri akimalizia krosi ya Tepsie.

Kwa ushindi huo Azam wamepanda juu kwa nafasi nne, kutoka nafasi ya 11 mpaka nafasi ya saba katika jedwali la msimamo wa ligiwakikusanya jumla ya alama 7 wakiwa wameshuka dimbani michezo mitano.

Geita Gold wamejikuta mpaka katika nafasi ya 14 baada ya kipigo hicho kutoka kwa Azam FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live