Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yaipigia hesabu kali Mtibwa Sugar

Ihefu Vs Azam FC Azam yaipigia hesabu kali Mtibwa Sugar

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Azam FC, Yusuph Dabo amesema kuwa wanafanyia kazi makosa ambayo yalitokea kwenye mechi zilizopita ili kupata matokeo kwenye mechi zijazo.

Novemba 24 Azam FC inatarajiwa kuwakabirisha Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU Novemba 19 ikiwa ni maandalizi kwa mechi zijazo ilipopata ushindi wa mabao 3-1.

Dabo amesema kuwa ushindani ndani ya ligi ni mkubwa hivyo wachezaji nao ni muhimu kuongeza umakini kwenye mechi zote.

“Makosa ambayo yamepita tunafanyia kazi ili kupata matokeo kwenye mechi zijazo ambazo zina ushindani mkubwa.Wachezaji wanatambua kwamba tunahitaji kupata ushindi.

“Kwa muda ambao tunakuwa nao kwenye mazoezi kuna maendeleo ambayo yanatokea na hilo linazidi kutupa nguvu kuelekea kweye mechi zetu zinazofuata,”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: