Klabu ya Azam FC imemaliza nafasi ya pili katika msimamo wa ligi Kuu Tanzania Bara na hivyo kuilazimisha Klabu ya Simba kumaliza nafasi ya tatu licha ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika Uwanja wa Mkapa dhidi ya JKT Tanzania.
Azam nayo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Geita Gold kwa mabao ya Fuentes Fei Toto na kumaliza nafasi ya pili kwa kujikusanyia alama 69 baada ya michezo 30, idadi sawa na Simba huku Azam ikiwa na faida ya mabao mengi ya kufunga.
Mabao ya Simba katika mchezo wa leo yamefungwa dakika za lala salama na Saido Ntibazonkiza dakika ya 88 kwa mkwaju wa Penati na Willy Somba Onana dakika ya 93.
Kwa mantiki hiyo Simba itashiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho mwakani sambamba na Coastal Union huku Mabingwa Yanga wakiungana na Azam FC kuiwakilisha nchi katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa.