Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yaichapa Coastal Union 1-0, wakwea kileleni kwenye msimamo

Azam Yaichapa Coastal Union 1 0, Wakwea Kileleni Kwenye Msimamo Azam yaichapa Coastal Union 1-0, wakwea kileleni kwenye msimamo

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Azam FC wamezima kelele za Coastal Union kwa kuwachapa goli 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Azam walikuwa ugenini CCM Mkwakwani jijini Tanga ambapo walipata bao pekee la mchezo kupitia kwa kiungo wao Feisal Salum 'Fei Toto'.

Azam wamekwea kileleni kwenye msimamo kwa kufikisha alama 13 wakiwa wamecheza michezo mitano wakifuatiwa na Simba wenye alama 12 wakiwa wamecheza michezo minne huku Yanga wakiwa nafasi ya tatu na alama zao 9 wakiwa wamecheza michezo minne.

Kabla ya mchezo huo, Coastal Union walitamba kuwa wamejiwekea mkakati wa kushinda michezo yote ya nyumbani kwa operesheni yao waliyoiita operesheni kata ngebe lakini matokeo yake leo wamekatwa wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live