Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yahamishia nguvu huku

Azam FC Ratba Bara Azam FC

Sun, 2 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupoteza matumaini ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu huu, Azam FC imehamishia nguvu zake kwenye mashindano ya Azam Sports Federation Cup.

Aprili 3, mwaka huu, Azam itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar, ukiwa ni mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Akizungumza nasi, Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe, alisema kuwa wanatambua umuhimu wa mashindano hayo na kila kitu kipo vizuri.

“Timu kubwa inafanya vitu vikubwa na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zake, hivyo nasi tunajipanga kufanya mambo makubwa kwa kupata matokeo mazuri.

“Safari hii tumedhamiria kufanya kweli kwenye Kombe la Azam Sports Federation, ndio maana tulianza kupata ushindi mkubwa kwenye mechi zile za mwanzo, ikumbukwe tuliwafunga Malimao mabao mengi,” alisema Ibwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live