Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yafunguka kumuuza Kipre Jr Simba SC

Kipre X Zaka Azam yafunguka kumuuza Kipre Jr Simba SC

Sat, 9 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Azam, Zakaria Thabiti maarufu kama Zakazakazi amefunguka kuhusu tetesi za zklabu ya Simba kumtaka winga wao, Kipre Jr ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa mwiba kwelikweli kwenye lango la mpinzani.

Akiongea baada ya ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya KMC, Zaka amesema kama kweli wanamtaka wanatakiwa kuwa na vijana wadogo wenye miaka 22, yaani wachezaji 25 ndiyo sawa na Kipre JR mmoja.

Zakaria amesema hata Real Madrid ya Ligi Kuu ya Hispania wenyewe pia walimtamani Kipre Jr lakini wameshindwa kumpata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live