Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yaendelea kusuasua

A697428ed51b4b02232b8fb8dbc1b275 Azam yaendelea kusuasua

Tue, 1 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MATOKEO ya ushindi yameendelea kuwakalia kushoto timu ya Azam FC, baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Biashara United mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume Mara jana.

Azam wamepata sare hiyo huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza pointi sita kwenye michezo miwili iliyopita wakianza kufungwa na KMC bao 1-0 kabla ya kupata matokeo kama hayo dhidi vinara wa Ligi, Yanga.

Azam licha ya kufanya mabadiliko kwenye benchi lao la ufundi kwa kumuondoa aliyekuwa kocha wao Mkuu Aristica Cioaba wiki iliyopita, bado hawajapata ushindi, kwani kuwa wakati wachezaji wao wanaonekana kutojituma uwanjani.

Katika mchezo huo dhidi ya Biashara, Azam walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 20 kupitia kwa Ayoub Lyanga wakati Biashara walisawazisha kipindi cha pili dakika ya 59 kwa bao la Timothy Omwenga.

Matokeo hayo yanawafanya Azam kuendelea kukalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi 26 baada ya kushuka uwanjani mara 13 sawa na wapinzani wao Biashara wanashika nafasi ya saba na alama 18.

Katika mchezo huo ulianza kwa kasi kwa kila timu kucheza kwa kuzidisha umakini hususani eneo la ulinzi, lakini Azam walionekana kuwa bora zaidi kwa kutengeneza nafasi kutoka sehemu ya kiungo hali iliyowanufaisha kwa kwenda mapumziko wakiwa kifua mbela kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa kila kikosi kufanya mabadiliko ambayo yalionekana kubadilisha mazingira ya mchezo kwa kushambuliana kwa zamu.

Chanzo: habarileo.co.tz