Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam wawekewa Sh500 milioni waichape Yanga

Azam Vs Art Solar 7 Wachezaji wa Azam FC

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Azam FC leo Jumatatu itakuwa mgeni wa Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu mzunguko wa sita mechi itakayochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na tayari mastaa wa matajiri hao wa Chamazi wametengewa kitita cha fedha mezani kama watashinda mechi hiyo.

Mwanaspoti limepenyezewa na mmoja wa viongozi wa juu wa Azam (jina tuna-lo), tajiri wa kikosi hicho Yusuph Bakhre-sa ametenga zaidi ya Tsh 500 milioni kwa timu hiyo kama itaifunga Yanga.

“Miongoni mwa mechi muhimu kwetu ni pamoja na hii ya Yanga. Tunataka kushinda ili kuendelea kukaa juu kwenye msimamo.

“Na nikuambie, kila mtu ndani ya timu anaitaka mechi hii, tajiri tayari ameahidi zaidi ya Tsh 500 milioni kwa wachezaji na benchi la ufundi kama tutashinda, unaona ni mechi rahisi?” alisema kiungozi huyo.

Hata hivyo, Azam imekuwa ikikutana na ugumu dhidi ya Yanga katika mechi tano, Wanachamazi hao wameambulia sare moja tu kufungwa nne.

Azam FRC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na alama 13 baada ya mechi tano, huku Yanga ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 12 na nafasi ya kwanza ipo Simba yenye alama 15 baada ya michezo mitano.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: