Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam wawazima mdomo Yanga, wawachapa 2-1

Yanga Vs Azam 2 0 FT.jpeg Azam wawazima mdomo Yanga, wawachapa 2-1

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Azam FC wametoka kifua mbele ya Yanga SC kwa ushindi wa goli 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC.

Mbungi ilikuwa live katima Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar ambapo Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wao Clement Mzize katika kipindi cha kwanza dakika ya 10 ya mchezo.

Hata hivyo goli hilo la Yanga halikudumu muda mrefu kwani dakika chache baadaye dakika ya 19, Gibril Sillah alisawazisha na ngoma ikaenda mapumziko matokeo yakiwa ni 1-1.

Kipindi cha pili Azam walikuja na moto na kufanikiwa kupata bao la pili lililowekwa kimiani na Feisal Salum 'Fei Toto' dakika ya 51 ya mchezo ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo.

Azam wamefikisha alama 47 baada ya ushindi huo wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo huku Yanga wakiongoza msimamo wakiwa na alama 52. Hata hivyo, Azam wamecheza michezo 21 huku Yanga akiwa amecheza michezo 20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live