Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam watinga Fainali ngao ya Jamii, Yanga au Simba nani kumfuata?

Azam Waleeeeeee Azam watinga Fainali ngao ya Jamii, Yanga au Simba nani kumfuata?

Thu, 8 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Mcolombia, Jhonier Blanco ameanza kufungua akaunukurasa wa mabao ndani ya kikosi hicho baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa timu hiyo wa 5-2, dhidi ya Coastal Union.

Nyota huyo aliyesajiliwa na matajiri wa Dar es Salaam akitokea Aguilas Doradas, ameifungia bao timu hiyo dakika ya 45, katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii iliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Itakumbukwa msimu uliopita nyota huyo akiwa na kikosi cha Fortaleza CEIF iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza kwao Colombia, (Categoría Primera), aliyoichezea kwa mkopo akitokea Aguilas Doradas, alikuwa mfungaji bora baada ya kufunga jumla ya mabao 15.

Mabao mengine ya Azam FC katika mchezo huo yamefungwa na Gibril Sillah dakika ya 13, Feisal Salum 'Fei Toto' dakika ya 39 na nyota wapya wa kikosi hicho Adam Adam aliyetokea Mashujaa akipachika la nne dakika ya 87 na Ever Meza akiweka msumari wa mwisho dakika ya 90.

Kwa upande wa mabao ya kufuatia machozi kwa Coastal Union, yamefungwa na kiungo nyota wa kikosi hicho, Semfuko Charles dakika ya 26 na Abdallah Hassan dakika ya 86.

Ushindi wa Azam dhidi ya Coastal Union unaifanya timu hiyo kutinga fainali yake ya saba kati ya 19, zilizochezwa tangu mwaka 2001.

Hata hivyo, licha ya fainali hizo zote ila timu hiyo imenyakuwa ubingwa wa mashindano hayo mara moja tu ambapo ilichukuwa mwaka 2016, wakati ilipoifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1, baada ya miamba hiyo kutoka sare ya kufungana kwa mabao 2-2.

Azam inasubiri mshindi atakayecheza naye fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba ambazo zinapambana kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa Coastal Union, pia inasubiri timu itakayopoteza mchezo kati ya Yanga na Simba ili kucheza naye kutafuta mshindi wa tatu ambapo mechi hiyo na ya fainali zitapigwa Jumapili ya Agosti 11, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 9:00 Alasiri na saa 1:00 usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live