Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam wasikitika Robertinho kuondolewa Simba SC

Azam X Ibweee Azam wasikitika Robertinho kuondolewa mapema

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Simba kutangaza kuachana na aliekuwa Kocha wake Mkuu mbrazil Roberto Oliviera "Robertinho".

Klabu ya Azam FC imeonesha masikitiko yake huku wakionekana kutaka kufanya kile walichokifanya Yanga.

Akizungumza Afisa Habari wa Azam FC, Hashim Ibwe anasema

"Sisi kama Azam kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba Sc tulikuwa tunamtaka kocha huyo (Robertinho) aendelee kuwepo kwa kuwa tumezoea kuchukua alama tatu kwake, tunasikikltika sana kwa kuondokewa kabla ya muda "

" Kwasasa Azam Fc ipo kwenye safari ya kuusaka ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara 2023/2024 , bado wana imani na kocha wao Yusuf Dabo na kwamba hatuna mpango wa kuachana na kocha wetu "

Chanzo: www.tanzaniaweb.live