Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam wana ishu na Yanga

Azamfcofficial 20210824 8 002 Azam FC, wakendelea na maandalizi ya Oktoba 30

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina amesema kwa sasa malengo yao ni kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kuondoshwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Azam imerejea juzi nchini ikitokea Misri ilikofungwa bao 1-0 na Pyramids FC na kuondoshwa kwenye michuano hiyo na imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa.

“Upungufu uliojitokeza umetupa funzo kuelekea michezo yetu ijayo, naamini kutokana na ushiriki huu tumepata mwanga wa kikosi changu kufanya vizuri,” amesema.

Ameongeza kuwa mchezo wao na Yanga huwa mgumu siku zote ila wamejiandaa vyema kuibuka na ushindi baada ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo uliopita dhidi ya Namungo.

“Ninachokifanya ni kuwapa wachezaji wangu mbinu za kuwa na mwendelezo wa matokeo mazuri, kila timu imejipanga hivyo lazima kukabiliane na changamoto za aina yoyote,” amesema.

Winga mshambuliji wa timu hiyo Idd Seleman ‘Nado’ amesema kuwa kutolewa kwao kumewaongezea ari na hamasa ya kupambana zaidi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz