Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam wamkana Nasreddine Nabi

Hasheem Ibwe Nabi Kaimu Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Afisa habari wa klabu ya Azam Hashim Ibwe amezungumza leo kua klabu hiyo haijafanya mazungumzo yeyote na kocha wa Yanga Nasserdine Nabi.Ili kujiunga na klabu hiyo ya majiri wa Dar-es-salaam.

Ikumbukwe klabu ya Azam imemfukuza aliekua kocha wake mfaransa Lavagne ambae alidumu klabuni hapo kwa siku takribani 47 tu.

Wakati huohuo kocha wa Yanga Nabi tetesi zilikua zinasema amekaribia kufukuzwa klabuni hapo hivo Azam wakawa wanahusishwa nae.

Kufuatia hali hiyo imemfanya Hashim Ibwe kufunguka kua klabu hiyo haikua na mpango wa kuchukua kocha huyo ambaye bado yupo kwenye timu yake pia akiwa na mkataba hivvo wao kama Azam wapo kwenye hatua za kutafuta kocha mwingine lakini kwasasa timu itaendelea kua chini ya kocha Badru pamoja na mchezaji mkongwe klabuni hapo Agrey Morris.

Wakati huohuo Hashim Ibwe amewasisitiza Mashabiki wa Azam wajitokeze uwanjani siku ya kesho kuipa nguvu timu yao iwe inaenda kukabiliana klabu ya Simba.

Mchezo unaotarajiwa kua mgumu kwani Azam haijapata matokeo mazuri siku za karibuni wakati huo pia Simba inahitaji kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live