Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam wametengeneza zimwi lao litakalowatisha mpaka wahenga

Azam X Ibweee Azam wametengeneza zimwi lao litakalowatisha mpaka wahenga

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hivi tunawazingatia Azam FC au ndio tumechagua kucheza biti la vilabu kongwe vya Kariakoo. Ndio wameshikilia usukani wa soka la Tanzania ila Wana ramba-ramba naona wanakuja na tumaini jipya la kutengeneza zimwi lao la ubora.

"Wahenga waliwah sema kuwa zimwi likujualo halikuwi likakwisha" basi naona Azam wameamua kuisha na kutaka kutengeneza zimwi lao litakalotesa zaidi ya zimwi la Wahenga ambalo ni zimwi la kibisa.

Kuna kitu cha tofauti sana Azam msimu huu wanakionyesha ingawa misimu yote huwa wanaanza hivi ila kwa sasa hivi, wanaonyesha kuwa wana kitu cha tofauti zaidi kwenye kila eneo ili kusimika zimwi lao litakalokimbizana na mapacha wa Kariakoo kwenye miungu ya soka la Tanzania.

Miongoni wa nadharia iliyokuwa inaniumiza sana ni ile inayosema mpira pesa ila nikiwangalia Azam na safari yao ya kujipambania kuwa bora inagonga mwamba mbele ya mapacha.

Ubora wa Azam nausemea kwenye maeneo mengi uwanjani, kuanzia squad yao inawachezaji ambao wapo kwenye form bora, benchi la ufundi na maeneo mengine ya kiutendaji ingawa bado idara yake ya habari inasinzia sana wakati huu?

Huu ndio muda wa kuwapa morali wachezaji kupitia social media na kuisemea zaidi klabu juu ya ubora wao kwa sasa.

Ibwe na Zaka propaganda ambazo huwa wanazipa airtime pindi ambapo klabu huwa imefanyiwa dosari na waamuzi ni vema wangekuwa wanazitumia kwa nyakati kama hizi ambazo klabu yao imekuwa kwenye kilele cha ubora wao.

Uwezo wa wachezaji unashawishi kuvaa jezi ya Azam na kujinadi kuwa chama langu Azam na hakuna mtu atakaye kuhoji?

Irish novelist Darren O`shaughnessy aliwahi sema kuwa "Kwenye maisha kuna baadhi ya mambo kamwe huwezi kuyaelewa hadi na wewe uyapitie".

C E O POPAT baada ya kupitia mda mrefu msukumo wa kuiona Azam itakayokuwa kwenye kilele cha ubora basi amepata suluhisho ambalo litampa tabasamu la kusahau maumivu yaliyopita ingawa sio rahisi kama hesabu za matrix kwa PCM takers.

Michezo yao ya mwezi wa 11 wameshinda mechi 3 sawia na magoli 11 na cleansheet 2 kisha wakiruhusu bao 1.

Takwimu zao sawia na uwiano wa performance yao kwangu sio suprise kwani wanahitaji kuwa na twakwimu bora zaidi ya hizi. Wana Bank of quality players.

Ibwe& Zaka, Idara imelala!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live