Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam wajilaumu wenyewe - Mchambuzi

Azam FC Squad Azam wajilaumu wenyewe - Mchambuzi

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka nchini, Salama Ngale amesema, klabu za Azam na Coastal Union haziepukiki lawama kwa kutolewa mapema katika michuano ya kimataifa kutokana na kutojua vyema kutumia viwanja vya nyumbani.

"Timu ni lazima iangalie malengo yake ni yapi, kwa mfano ukiangalia Azam inahukumiwa kwa sababu ya matokeo yake ya kutoridhisha nyumbani, Coastal ilipata faida ya kuanzia ugenini, lakini ilipoteza mabao 3-0, ambayo ni mengi japo iliporudi nyumbani utakumbuka ilipata penalti dakika ya tano tu na ikakosa," amesema Salama.

Ameongeza, timu inapoenda katika mashindano hayo ni lazima iangalie malengo iliyojiwekea kwani kitendo cha miamba hiyo kutolewa mapema sio kigezo cha kuepuka lawama, kwani zipo klabu ambazo zimefanya makubwa ambayo hayakutarajiwa.

"Tumeshuhudia matokeo ya kuchukiza sana kwa mfano UD Songo na Simba na Jwaneng Galaxy na Simba pia, timu ikijipanga na kutambua malengo yake inaweza kupata kile ilichokikusudia, hivyo Azam na Coastal Union haziepuki lawama," amesema Salama.

Salama ameyabainisha hayo leo Agosti 28, 2024 wakati akichangia mada katika Mwananchi Space, inayoandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) yenye mada isemayo; Tumekosea wapi timu nne za Tanzania kutolewa mashindano ya klabu Afrika?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live