Klabu ya Azam FC inatakiwa kujifunza kwa Al Ahly, Wydad Casablanca, Esperence De Tunis, Siyo Azam FC ijifunze kwa Simba au Yanga.
Simba na Yanga ndiyo zile zile tu, Makundi Yanga kuachana na msimu huu mara ya mwisho waliingia group stage mwaka 1998, Simba mara ya mwisho kuingia Nusu Fainal michuano ya kimataifa ilikuwa mwaka 1993.
Hizi klabu hazina historia ya kuifanya Azam FC wajifunze au wawe inspired kwa chochote, Azam FC kama wanahitaji kufika mbali basi role model wao wawe timu ambazo zimefanya makubwa Africa na tunapozungumzia kufanya mambo makubwa ni pamoja na kutwaa makombe siyo medali shingoni.
Team hazina miondombinu, timu hazina usafiri wa kueleweka, team bado zinadhaminiwa kwa pesa za masimango sasa, mnataka Azam FC ijifunze kitu gani kwa Simba au Yanga.