Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam waitolea macho Kariakoo Derby

Azam Waitolea Macho Kariakoo Derby Azam waitolea macho Kariakoo Derby

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Shafii Dauda ameichambua mechi ya Yanga na Simba na kuonesha jinsi ambavyo Azam FC atakuwa akiitolea macho.

Kupitia ukurasa wake wa Instangam, Shafii ameandika hivi;

Kama Yanga itashinda #KariakooDerby maana yake inakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu lakini ikiwa Simba itashinda mchezo huo maana yake Yanga inakuwa imefungua tena milango kwa Simba na Azam kurudisha matumaini ya ubingwa.

Azam FC wapo pembeni lakini wanauangalia kwa hesabu kali mchezo wa #KariakooDerby kwa sababu bado wapo kwenye mbio za ubingwa lakini hata wakitolewa kwenye mbio za ubingwa wanaitaka nafasi ya pili ili msimu ujao wacheze Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa hiyo Azam FC imenusa harufu ya ubingwa lakini pia nafasi ya pili. Azam FC ina alama 50, tayari imecheza michezo 22 hadi sasa. Ikitokea Simba imefungwa na Yanga, tofauti ya alama kati ya Simba na Azam itakuwa ni nne huku Simba ikiwa imecheza michezo 21, Azam itaendelea kubaki nafasi ya pili.

Endapo Simba itashindwa kuifunga Yanga basi nafasi ya kuchukua ubingwa itabaki kuwa kwenye makaratasi lakini kwenye uhalisia itakuwa ngumu kutokea. Mbio za ubingwa zitabaki kwa Yanga na Azam.

Mchezo wa kiporo wa Simba vs Azam ndio utatoa picha ya timu itakayoweza kumaliza Ligi ikiwa nafasi ya pili ili kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live