Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam waishushia mvua ya magoli Kitayosce, Mwamuzi amaliza mechi

Fei Hatrick Fei Toto ametupia Mabao matatu kati ya manne ya Azam FC

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi Omary Mdoe aliyekuwa akichezesha mchezo kati Azam FC dhidi ya Kitayosce ameamua kumaliza mchezo kabla ya muda baada ya Wachezaji wawili wa Kitayosce akiwemo Golikipa kuumia, hivyo kufanya Kitayosce kubakiwa na wachezaji 6 tu uwanjani.

Awali Tabora United iliingiza wachezaji nane tu uwanjani ambao ndio waliokidhi vigezo vya kucheza mchezo huo. Mchezo ukiwa unaendelea wachezaji wao 2 waliumia hivyo wakasalia 6 hali iliyopelekea mchezo kushindwa kuendelea kwa mujibu wa kanuni ya 17 (31) ya Ligi Kuu timu ikiwa na wachezaji pungufu ya 7 mchezo hauwezi kuendelea

Hadi dakika ya 12 Azam walikuwa wanaongoza bao 4 kwa 0, mabao matatu yaliyofungwa na Feisal Salum huku moja likifungwa na Prince Dube.

Mpaka mchezo huo unamalizika, Azam FC 4-0 Tabora United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: