Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam waichapa Coastal Union dakika za Jioni Chamazi

Aakaminko James Azam waichapa Coastal dakika za Jioni Chamazi

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Azam FC wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo mtamu wa ‘funga nikufunge’, mabao ya Azam FC yamefungwa na James Akaminko dakika ya 56, Yahya Zayd dakika ya 70 na Iddi Nado dakika ya 90 na ushei, wakati ya Coastal Union yamefungwa na Maabad Maulid dakika ya 14 na Hamad Majimengi.

Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 32 katika mchezo wa 14 na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mechi mbili mkononi.

Coastal Union baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 12 za mechi 12 nafasi ya 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live