Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam wagumu kwa Simba tu

Djuma Shaban Azam FC.jpeg Azam wagumu kwa Simba tu

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miaka ya hivi karibuni Azam FC amekuwa kibonde pindi anapocheza na Yanga na Takwimu huwa zinaonyesha kuwa katika mechi 7 zilizopita Azam ameshinda mechi moja tu.

Katika mechi 7 hizo zilizopita,mechi ni upande wa Ligi Kuu ambapo Azam FC ameshinda mechi 1,sare mechi moja na kapoteza mechi 3.

Mechi nyingine mbili ilikuwa hivi Fainali ya FA,Azam FC alikufa goli moja na ile mechi ya Ngao ya Jamii pale Tanga alifungwa goli mbili. Kwa maana nyepesi Azam FC ni kibonde wa Yanga ila Azam FC amekuwa mbishi kwa Simba katika misimu hii miwili.

Tusubiri dakika 90 pale Benjamin Mkapa,Licha ya kuwa Azam FC ni mteja tu ila msimu huu hajapoteza hata mechi moja wakati Yanga wao wamefungwa mechi moja na Ihefu FC.

Takwimu zao Katika Dabi ya Dsm

1.Yanga 2-0 Azam Ngao ya Jamii 2.Yanga 1-0 Azam Fainali FA 3.Azam 2-3 Yanga Ligi Kuu 4.Yanga 2-2 Azam Ligi Kuu 5.Azam 1-2 Yanga Ligi Kuu 6.Yanga 2-0 Azam Ligi Kuu 7.Yanga 0-1 Azam Ligi Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live