Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam wafuta uteja kwa Simba, watia doa rekodi ya Mgunda

Azam Vs Simba FT Azam 1-0 Simba SC

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yametimia. Dakika 90 za Dabi ya Mzizima zinakamilika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara umewashuhudia Azam FC wakifuta uteja wa zaidi ya miaka mitano na kufanikiwa kuibuka na alama tatu wakiichapa Simba goli 1-0 lililofungwa kipindi cha kwanza dakika ya 35 na Prince Dube.

Mbali na Ushindi huo kuvunja mwiko wa Azam kutoshinda dhidi ya Simba kwa muda mrefu, vile vile umetia doa katika rekodi za Kocha wa Simba Juma Mgunda ambae tangu alipokabidhiwa timu hiyo akirithi mikoba ya Zoran Maki alikuwa hajapoteza mchezo wa Ligi wala Kimataifa.

Ushindi huo wa Azam unawasogeza mpaka nafasi ya 4 katika jedwali la msimamo wa Ligi wakiwa na alama 14 baada ya kucheza michezo 8 sawa sawa na Simba waliopo nafasi ya tatulakini wakiwa wameshacheza michezo 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live